Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’, ameonesha kushangazwa na kuumizwa na taarifa zinazosambaa kuwa amepewa pesa ili ataje watu au ajitangaze, jambo ambalo si la kweli kwa upande wake na anachukulia wavumishi hao kama watu wenye wivu wasiomtakia mema na wanaotaka kumuona akiendelea kutaabika kwenye matumizi ya dawa hizo.
‘TID’ amehaidi kuwachukulia hatua watu wanaosambaza taarifa kuwa amepewa pesa na Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kama kivuli katika sakata la dawa za kulevya.
” Watu wanaushahidi gani kama mimi Mh. Makonda kanipa pesa au wanazungumza tu ? mimi nataka huyo sijui Steve nani nani aseme kwamba aliniona nikiwapatia hizo pesa bila hivyo mimi nitamshtaki, anaituhumu serikali, bila ushahidi, hili ni kosa ambalo naweza nikampeleka mtu mahakamani” amesema Top In Dar (TID).
TID ameonesha kuumizwa na uvumi huo kwani anaamini yeye kuchagua njia sahihi sio makosa, ni kweli alikuwa muathirika wa dawa za kulevya na ameamua kuachana nazo na anaishukuru Serikali kwa kumpa sapoti ya kuachana na dawa za Kulevya pamoja na kumpa nafasi ya kuelimisha vijana wenzake ambao bado wapo katika janga.