Mume na mke wamefariki dunia mara baada ya kufunga ndoa, gari aina ya Toyota Premio iliyokuwa  imebeba maharusi hao kusombwa na mafuriko katika daraja la mto Seliani majira ya saa nne usiku maeneo ya Ngaramtoni  jijini Arusha.

Dereva wa gari hiyo aina ya Toyota Premio, Yusuf Jacob alinusurika baada ya kushuka kutazama wingi wa maji lakini wakati anarejea kwenye gari alikuta tayari limezolewa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema watu saba wamefariki dunia kwa kusombwa na mafuriko katika matukio tofauti tofauti, wakiwemo mume na mke waliotoka kufunga ndoa.

Amewataja waliofariki kuwa ni maharusi, Munisi Loy, na mkewe Nebrise Mungaya mwenye umri wa miaka, na mama wa bwana harusi, Inoti George.

Katika tukio jingine, mtu mmoja Babu Loikeki alisombwa na mafuriko alipokuwa akivuka mto katika kijiji cha Kereiani na tukio la tatu ni la dereva wa bodaboda, Seuri Meseyeki ambaye alisombwa na mafuriko katika eneo la Orelian Ngaramtoni.

 

TID ataka kuwashtaki waliomtuhumu kahongwa na Makonda
Baada ya kuzushiwa kifo, Mwinyi awatoa hofu Watanzania