Wanasheria wa kujitolea wa Mkoa wa Dar es salaam, walioitikia ombi la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda wa kuwataka wanasheria hao kuwasaidia wananchi wa Mkoa huo kuhusu mambo ya kisheria wamekabidhi taarifa ya utendaji wa kazi hiyo kwa kipindi cha kuanzia 16/12/2016hadi 24/2/207.
Aidha, akiwasilisha taarifa hiyo kiongozi wa wanasheria hao, Georgia Kamina amesema kuwa wamehudumia wananchi 10217 na jumla ya kesi kesi 701 zimeweza kusikilizwa zikiwemo za migogoro ya ardhi, kazi, mirathi na ndoa, pamoja na kushugulikia migogoro sugu iliyokaa zaidi ya miaka kumi na sasa imekwisha.
‘’Moja ya kesi ambayo ilitutia changamoto ni kesi ya mirathi ambayo faili la kesi hiyo lilipotea nashukuru mungu tulifuatilia hadi faili hilo lilipatikana kesi hiyo ilidumu kwa muda wa miaka kumi na mama huyo mjane alipata haki yake,’’ amesema Kamina.
Ameongeza kuwa changamoto kubwa iliyopo ni wananchi wengi hawana uelewa kuhusu mambo ya kisheria hivyo nidhahiri kuwa wananchi wanahitaji msaada wa kisheria.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaa, Paul Makonda amewashukuru wanasheria hao kwa kazi hiyo nzuri waliyoifanya kuwa imetia hamasa kwa wanasheria wengine na kuwataka wanasheria kuiga kufanya kazi za kujitolea kuisaidia jamii katika matatizo ya kisheria.
‘’Mji huu unawajanja wengi na nchi yetu si wote tulibahatika kwenda shule wajanja hutumia fursa hiyo kuwa kandamiza wengine nawashukuru sana wanasheria wote mlioshiriki katika kazi hii’’ amesema Makonda.