Ikiwa homa ya pambano la watani wa jadi ikizidi kupanda nchini kati ya Simba na Yanga, Msanii  maarufu wa Bongo Movies Jacob Steven ‘JB ‘ ambae ni shabiki wa kutupwa wa timu ya Simba ametamba kuwa kikosi chake hakiwezi kumuangusha kutokana na kuwa na washambuliaji wenye uchu ya kufunga

 Jacob Steven ‘JB’ ambaye amesema, Simba kwa sasa ipo vizuri sana katika safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Ibrahim Ajibu, Laudit Mavugo, pamoja na Juma luzio hivyo basi  Yanga lazima atasuburi kwa hawa watu watatu.

“Mimi naona hiyo mechi tunamfunga Yanga mabao mawili kwa bila huku wafungaji wakiwa ni vijana wanaojituma ili kurudisha heshima ya klabu yetu Simba ambao ni Ajibu na Mavugo,” amesema JB.

Aidha, muigizaji huyo amewambia wapenzi wa Simba kuwa mwaka huu kombe la Ligi kuu Tanzania bara linaenda mitaa ya Msimbazi hivyo wawasapoti vijana wao katika mazuri ambayo wanayafanya na pia umoja ndiyo ushindi wa timu hiyo.

 

Trump apiga marufuku baadhi vyombo vya habari kuingia Ikulu ya Marekani
Wanasheria wa kujitolea wakabidhi ripoti kwa Makonda