Uongozi wa klabu ya Deportivo La Coruna umetangaza kumfuta kazi Gaizka Garitano, baada ya kikosi chao kukubali kufungwa mabao 4-0 dhidi ya Leganes mwishoni mwa juma lililopita.
The Galicians, wametangaza maamuzi hayo yanayokwenda sambamba na kuchoshwa na meneja wa meneja huyo, ambaye hakuwahi kushinda mchezo wowote tangu mwezi Disemba mwaka jana kwa kuhofia huenda wangeendelea kupata matokeo mabovu.
Tangu mwezi Disemba mwaka jana kikosi cha Deportivo La Coruna kimekubalia kufungwa michezo mitano mfululizo.
Gaizka Garitano
Kwa sasa Deportivo La Coruna inakamata nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi ya nchini hispania, ikiwa na point mbili juu ya Sporting Gijon wanaoshika nafasi ya 18, huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo imeeleza kuwa, meneja wa kikosi cha akiba Cristobal Parralo atakuwa msimamizi wa mazoezi ya kikosi cha kwanza, na huenda akakaimu nafasi ya kukaa kwenye benchi la ufundi, mpaka hapo uongozi wa Deportivo La Coruna utakapomtangaza meneja mpya.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Hispania, meneja anaetajwa kuchukua nafasi ya Gaizka Garitano ni Pepe Mel ambaye aliwahi kuvinoa vikosi vya klabu za West Bromwich Albion na Real Betis.