Jeshi la Korea kusini limesema kuwa Korea kaskazini imerusha makombora katika bahari ya Japan, Jeshi la Korea kusini limesema kuwa makombora hayo yamerushwa kutoka kwenye eneo la Tongchang-ri lililopo kwenye mpaka kati ya Korea kaskazini na China na kurushwa kwa umbali takriban kilomita elfu moja

Akiongea na Waandishi wa Habari, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe amesema makombora hayo yanadhihirisha ushahidi tosha wa vitisho vipya kutoka kwa Korea kaskazini.

”Korea kaskazini imefyatua makombora yake manne leo na kuangukia karibu na eneo letu la maji lenye manufaa kwetu kiuchumi,” amesema Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe.

Japan inaipinga Korea kaskazini kurusha makombora kwa kuwa nchi hiyo inaonekana kuwa ni tishio, Japani imesema kuwa itafuatilia tukio hilo ili iweze kujua chanzo cha kurusha makombora hayo.

JPM aagiza Dangote apewe eneo la kuzalisha makaa ya mawe
FBI yapinga madai ya Trump kuhusu Obama