Mkurugenzi wa shirika la kijasusi la FBI, James Comey amekana madai ya rais Donald Trump kwamba aliyekuwa rais wa taifa hilo Barrack Obama alifanya udukuzi wa simu zake kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

Comey  amelitaka shirika la haki nchini humo kukataa madai hayo kwamba Obama aliagiza uchunguzi wa simu za Donald Trump wakati wa kampeni za uchaguzi uliokwisha.

Aidha, Vyombo vya habari nchini Marekani viliwanukuu maafisa wakisema kuwa, Comey anaamini hakukuwa na ushahidi kuthibitisha madai ya Trump.

Hata hivyo, Rais huyo wa Marekani kupitia Chama cha Republican, anakabiliwa na uchunguzi kuhusu uingiliaji wa Urusi ili kuunga mkono uchaguzi wake hajatoa ushahidi wowote kuunga mkono madai yake kwamba simu zake katika ofisi ya Trump Tower zilidukuliwa.

Korea ya Kaskazini yarusha makombora Japan
Video: Makonda atokwa machozi Kanisani, Magufuli aipa siku 7 Wizara ya Nishati