Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), leo linatarajia kuweka hadharani deni la sh. bilioni 121 inazowadai Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
Kauli hiyo imekuja siku chache baada Rais John Magufuli kuliagiza Shirika hilo kuikatia umeme Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar SMZ baada ya kushindwa kulipa deni hilo kwaajili ya kusambaza umeme visiwani humo.
Rais Magufuli alitoa kauli hiyo wakati wa kuweka jiwe la msingi katika kituo cha kupooza umeme wa kilovoti 132 kilichopo Mkoa wa Mtwara wakati wa ziara yake aliyoifanya hivi karibuni.
Aidha, Ofisa Habari na Uhusiano wa Tanesco, Leyla Muhaji  amesema kuwa shirika haliwezi kukaa kimya kwa sababu suala hilo teyari Rais Magufuli ameshalingumzia.
“Mimi na viongozi wenzangu tutajipanga tuweze kutoa mchanganuo wa deni lenyewe lilivyoanza hadi lilipofikia, kwa sasa tupo safarini tutakaporejea tutaweza kutoa taarifa sahihi,”amesema Muhaji.
Amesema kuwa wataandaa taarifa ya deni hilo ambayo itatolewa kwa vyombo mbalimbali vya habari, ili viweze kutoa habari kwa wananchi na kuondoa mkanganyiko uliopo.
Hata hivyo, Rais Magufuli alisema wadaiwa sugu wakatiwe umeme kwa vile shirika hilo halipo kisiasa, hivyo wadaiwa wote wanapaswa kulipa madeni yao na watakao shindwa wakatiwe umeme hata kama ni Ikulu.

Nicolas Nkoulou Ajiweka Pembeni
Arsenal Ya Arsene Wenger Kupindua Matokeo Leo?