Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amemshukia Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe, ambaye anataka kufuta jina lake kwenye orodha ya wagombea urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Lissu amesema kuwa yeye ni mgombea halali wa nafasi hiyo na kwamba kauli ya Mwakyembe haitabadilisha chochote kuelekea uchaguzi huo unaotarajiwa  kufanyika Machi 18 mwaka huu.

“TLS haitegemei Serikali kwa namna yeyote ile katika kuendesha mambo yake ambapo uhuru huo unatambuliwa na sheria za Tanzania na mkataba wa kimataifa ambayo Tanzania ni mwanachama,”amesema Lissu.

Aidha, Lissu amesema kuwa endapo Waziri Mwakyembe ataendelea kuingilia uchaguzi huo, TLS haitakuwa na haki ya kujiita chombo huru kinachojitegemea.

Hata hivyo, Lissu amewataka wanachama wa TLS kupinga na kupiga vita unyanyasaji huo kwenye uhuru wa kitaaluma, na kuongeza kuwa huu ni wakati wa kujitathmini na kutathmini nafasi yao katika jamii.

Bob Arum: Khan Hatakua Mpinzani Wa Manny Pacquiao
Kifimbo Cha Malkia Kufika Tanzania