Baada ya Askofu Josephat Gwajima kutumia zaidi ya wiki tatu kuzungumzia suala la dawa za kulevya na elimu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa madai kuwa ametumia cheti cha mtu, ndugu wa kiongozi huyo wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ameibuka na kumshambulia akimtaka aache mamlaka husika zifanye kazi yake.
Mwanasheria Methusela Gwajima ambaye ni mdogo wake Askofu Gwajima ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo, amehoji kuwa kwanini suala la elimu ya Makonda limeibuliwa wakati huu ambapo amevalia njuga suala la vita dhidi ya dawa za kulevya
Amesema kuwa wanaozungumzia elimu ya Makonda hawakupaswa kufanya hivyo bali walitakiwa kuunga mkono vita ya dawa za kulevya. na kuhoji kuwa walikuwa wapi kipindi kile kabla kuongelea vyeti kabala Makonda kuanzisha vita dhidi ya dawa za kulevya.