Baada ya Askofu Josephat Gwajima kutumia zaidi ya wiki tatu kuzungumzia suala la dawa za kulevya na elimu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa madai kuwa ametumia cheti cha mtu, ndugu wa kiongozi huyo wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ameibuka na kumshambulia akimtaka aache mamlaka husika zifanye kazi yake.

Mwanasheria Methusela Gwajima ambaye ni mdogo wake Askofu Gwajima ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo, amehoji kuwa kwanini suala la elimu ya Makonda limeibuliwa wakati huu ambapo amevalia njuga suala la vita dhidi ya dawa za kulevya

Amesema kuwa wanaozungumzia elimu ya Makonda hawakupaswa kufanya hivyo bali walitakiwa kuunga mkono vita ya dawa za kulevya. na kuhoji kuwa walikuwa wapi kipindi kile kabla kuongelea vyeti kabala Makonda kuanzisha vita dhidi ya dawa za kulevya.

Aidha, Mwanasheria huyo ametahadharisha kuwa kama vita dhidi ya dawa za kulevya itashindwa, huenda asiibuke mtu mwingine mwenye ujasiri kama Makonda kwa sababu kila mmoja atakuwa anahofia kufanyiwa kama alivyofanyiwa Makonda.
Hata hivyo, Methusela amemshambulia kaka yake Askofu Gwajima kwa kugeuza suala la dawa za kulevya na elimu ya Makonda kuwa sehemu ya mahubiri kanisani kwake.

Lissu: Hatutakubali uchaguzi wa TLS usitishwe
JKCI yashauri watanzania kuandika wosia wa kuchangia viungo