Baadhi ya wagombea wa nafasi ya  urais kupitia kwa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika TLS wanatarajia kuwasilisha maombi ya kujumuishwa kama wadaiwa katika kesi ya kupinga kufanyika kwa uchaguzi wao uliopangwa kufanyika tarehe 18  ya mwezi huu.
Wamefikia hatua hiyo ili kuongezea nguvu upande wa wadaiwa kufuatia kesi iliyofunguliwa na wanachama wawili wa chama hicho ambao wamefungua kesi katika Mahakama kuu kupitia Mkoa wa Dodoma na Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,  mgombea Urais wa chama hicho, Tundu Lissu amesema uchaguzi huo umekuwa ukifuatiliwa kwa karibu na watu wengi huku akibainisha kuwa kuna kile alichokiita njama dhidi ya kuharibu uchaguzi huo
Aidha, Lissu ameongeza kuwa wanachama wa chama hicho hawatakuwa tayari kuona uchaguzi unasitishwa kutokana na sheria za chama hicho, na kusisitiza kufanyika kwa uchaguzi wa chama hicho ambacho amedai kimekuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya sheria nchini.
Katika kesi ya msingi ya kupinga uchaguzi huo iliyofunguliwa na wanachama hao, washtakiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na chama chenyewe (TLS).
Kwa upande wake mgombea mwingine wa nafasi ya urais ambaye aliwahi kuwa Waziri wa mambo ya ndani, Lawlence Masha amesema kuwa chama chao hakina kipengele chochote kinachozuia wanasiasa kugombea nafasi ya uongozi katika chama hicho, huku akiwataka wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkuu wa chama hicho ambao unatarajiwa kufanyika mkaoni Arusha  tarehe 18 ya mwezi huu.

Tanesco yaanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli, yatoa wiki mbili kwa wadaiwa sugu
Video: Mdogo wake Askofu Gwajima awataka Watanzania wasipotoshwe na Askofu Gwajima