Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye ameiomba Serikali kusimamia misingi ya demokrasia katika kutatua malalamiko ya wananchi na kusimamia ustawi wa jamii ya Watanzania.
Ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, amesema kuwa kama Serikali itafanyia kazi malalamiko na mapendekezo yanayotolewa na wananchi ni wazi taifa litafikia malengo yake liliyojiwekea ya kupunguza hali ya umasikini na kuongeza pato la taifa kwa ujumla.
“Taifa letu litasonga mbele kama Serikali itakuwa inafanyia kazi mapendekezo yanayotolewa na wananchi na kutatua kero zao,”amesema Sumaye
Aidha, Sumaye amewaasa watendaji wa Serikali kutumia vizuri misaada inayotolewa na nchi wahisani ili kuhakikisha fedha za wananchi zinazotumiwa katika ulipaji wa madeni zinafanya kazi iliyokusudiwa.
Hata hivyo, ameongeza kuwa kama Serikali itatumia vizuri rasilimali zilizopo nchini, basi wananchi watanufaika na kuondokana na umasikini uliokisili na kuleta manufaa kwa Watanzania wote hasa wale wasiofikiwa na huduma za kijamii.