Kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi kimeendelea kula msoto wa matokeo mabovu, licha ya kumtimua Danny Blind kwenye benchi la ufundi mwishoni mwa juma lililopita.
Uholanzi imeendelea kupoteza katika michezo yake ya kimataifa, baada ya kukubali kufungwa na Italia usiku wa kuamkia leo chini ya kocha wa muda, Fred Grim.
Mchezo huo wa kirafiki ambao ulitarajiwa kuwa na matokeo tofauti kwa Uholanzi, ulimalizika kwa Italia kupata ushindi wa mabao mawili kwa moja.
Hata hivyo, Uholanzi walikua wa kwanza kupata bao kupitia kwa Alessio Romagnoli wa Italia aliyejifunga mwenyewe, kabla ya Eder na Leonardo Bonucci hawajaifungia The Azzuri mabao mawili ya ushindi.
Mchezo huo ulikua unafuatiliwa na aliyekua kocha wa Uholanzi wakati wa fainali za kombe la dunia 2014 Louis Van Gaal ambaye alikua sambamba na kocha Fabio Capello wa Italia.
Mpaka sasa shirikisho la soka nchini Uholanzi halijatoa tamko lolote la kuwa katika mazungumzo ya kuziba nafasi ya Blind, ambayo inatakiwa kumpata mrithi ili kunusuru matokeo yanayokiandama kikosi cha The Orange.
Matokeo ya michezo mingine ya kimataifa ya kirafiki iliyochezwa usiku wa kuamkia hii leo.
Myanmar 0 – 1 India
Georgia 5 – 0 Latvia
Lebanon 2 – 0 Hong Kong
Albania 1 – 2 Bosnia-Herzegovina
Egypt 3 – 0 Togo
Estonia 3 – 0 Croatia
FYR Macedonia 3 – 0 Belarus
Urusi 3 – 3 Belgium
Afrika Kusini 0 – 0 Angola
Morocco 1 – 0 Tunisia
Cameroon 1 – 2 Guinea
Luxembourg 0 – 2 Cape Verde
Austria 1 – 1 Finland
Ireland 0 – 1 Iceland
Ureno 2 – 3 Sweden
Ufaransa 0 – 2 Hispania