Tanzania imepanda kwa nafasi 22 kwenye viwango vya ubora wa soka kwa mwezi Machi, kufuatia matokeo mazuri iliyoyapata katika michezo ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Botswana na Burundi.

Februari mwaka huu Tanzania ilikuwa nafasi ya 157 huku katika viwango vilivyotangazwa leo na FIFA ikikamata nafasi ya 135.

Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ iliifunga Botswana mabao 2-0 kabla haijaibutua Burundi 2-1 mwishoni mwa mwezi uliopita.

Brazil imeipiku Argentina katika nafasi ya kwanza huku Ujerumani ikishika nafasi ya tatu.

Serikali ya Morocco kukabiliana na athari ya mabadiliko ya Tabianchi
Yakubu Aiyegbeni Ashindwa Kutimiza Lengo