Uongozi wa klabu ya Coventry City umevunja mkataba na mshambuliaji kutoka nchini Nigeria Yakubu Aiyegbeni ikiwa ni baada ya miezi mitatu kupita, tangu aliporejea nchini England akitokea Uturuki.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu za Portsmouth na Everton zote za England alijiunga na The Sky Blues wakati wa dirisha dogo la usajili, na alisaini mkataba wa muda mfupi ambao ulitarajiwa kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Yakubu mwenye umri wa miaka 34, amecheza michezo mitatu tangu alipojiunga na Coventry na hajabahatika kufunga bao, na kwa sasa anasumbuliwa na maumivu wa misuli ya paja aliyoyapata wakati wa mchezo wa ligi daraja la kwanza dhidi ya Swindon Town walioibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja Februari 25.

Maamuzi ya Coventry City ya kuvunja mkataba na mshambuliaji huyo yamekuja kutokana na majeraha yake kutokua na matarajio ya kupona hadi mwishoni mwa msimu huu, hivyo wameona ni bora waachane nae katika kipindi hiki.

Botswana, Burundi Zaibeba Tanzania Viwango Vya Ubora
Majaliwa: Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kiuchumi