Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo dos Santos, amefikisha mabao 100 katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya na kumuacha mpinzani wake wa karibu kwa sasa Lionel Messi.

Ronaldo aliifungia Real Madrid mabao mawili katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali dhidi ya FC Bayern Munich, na kufikisha idadi hiyo ya mabao ambayo inamuweka katika historia ya kipekee.

Messi alitarajiwa huenda angefikisha idadi hiyo ya mabao kabla ya mchezo wa juzi dhidi ya Juventus FC, lakini hali ilikua tofauti, kufuatia kichapo kilichowaangukiwa FC Barcelona cha mabao matatu kwa sifuri.

Kabla ya mchezo huo, Messi alikua ana mabao 97 aliyofunga katika michezo ya nyuma ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ronaldo alianza kufunga mabao upande wa michuano ya klabu bingwa akiwa na Man Utd kabla ya kuhamia Real Madrid mwaka 2009.

Live: Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Real Madrid yaitungua Bayern 2-1