Mwamba wa Kaskazini, Joh Makini amewajibu wale wanaodai kuwa mtindo wake wa kughani unafanana na ule wa nguli wa hip hop raia wa Marekani, Jay Z.
Joh ambaye Jumamosi iliyopita alikuwa kwenye The Playlist ya 100.5 Times Fm, alikana kupita na mitambao ya Jigga. Hata hivyo, alieleza kufurahishwa na namna wanavyomfananisha na rapa huyo akidai kuwa wameona hakuna anayeweza kufananishwa naye zaidi ya Jay Z.
“Mimi nitasema tu, labda niambie kuna mstari gani wa Jay Z ambao nimetohoa, au hata kuchukua flow… sijawahi. Kwa sababu mimi naimba maisha ya Sinoni Daraja Mbili na Tanzania, yeye anaimba maisha ya Brooklyn na Marekani,” Joh alifunguka.
“Nafikiri niko katika level ambayo hawaoni mtu mwingine wa kunifananisha naye. Kwahiyo mimi naona poa, kama wananifananisha na Jay Z.. yeah I like it, kuliko ungenifananisha na mtu mwingine ambaye… You Know!”
Rapa huyo ambaye kwenye wimbo wake ‘Waya’ alisikika akijifananisha na Jay Z na rapa Russell Simmons, akirap ‘TZ Jay-Z Russell’, alisema kuwa katika mstari huo alimaanisha kuwa yeye ni mtafutaji kama marapa hao ambao walianzia katika maisha ya chini na mihangaiko mingi hadi kufikia mafanikio makubwa.