Sekta ya madini nchini imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi na shughuli mbalimbali za maendeleo kupitia uwekezaji, ikiwemo ujenzi wa miundombinu muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Aidha, Mchango wa makampuni umekuwa na tija kwa taifa kwa kutengeneza ajira pamoja na kulipa kodi zinazostahili kulipwa, kuchangia soko la fedha za kigeni, manunuzi ya huduma pamoja na michango ya hiyari kwa shughuli mbalimbali za maendeleo kwa jamii zinazozunguka makampuni hayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania ya mwaka 2015, inaonyesha kuwa sekta rasmi ya uchimbaji madini ilitoa ajira 7,355 ambazo ni za moja kwa moja  na zaidi ya ajira 3,000 kupitia makampuni ya wakandarasi.

Kwa upande wa kulipa kodi, taarifa hiyo inaonyesha kuwa kati ya mwaka 2009 na 2015 makampuni makubwa yamelipa kodi Serikalini zaidi ya shilingi billioni 870 ikiwa ni mrahaba  na zaidi ya shilingi billioni 680 zililipwa kama kodi ya mapato na kodi nyinginezo ambazo sio za moja kwa moja.

Hata hivyo, Uendeshaji wa sekta ya madini nchini upo chini ya Serikali na taasisi zake ambazo ni Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Shirika la Uchimbaji wa Madini la Taifa (STAMICO), ambapo sera zilizowekwa mwishoni mwa miaka ya 1990 ziliwavutia wawekezaji wageni ambao walianzisha migodi mikubwa ya uchimbaji wa dhahabu.

Video: Joh Makini Awajibu Wanaodai Anajifananisha na Jay Z
Mkurugenzi UNDP atimuliwa nchini