Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeliagiza Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya Maendeleo (United Nations Development Programs – UNDP) kwa upande wa Tanzania kumuondoa nchini Mkurugenzi wa Shirika hilo, Awa Dabo.

Aidha, Serikali imefikia uamuzi huo kutokana na Mkurugenzi huyo kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi ya Watumishi wenzake na Menejimenti ya Shirika hilo.

Maamuzi hayo yamefikiwa ili kunusuru kuzorotesha utendaji kazi wa shirika hilo nchini na kupunguza kasi ya kuleta maendeleo kwa Watanzania endapo hatua za haraka zisingechukuliwa.

Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje imetoa rai kwa UNDP kuwakumbusha Watumishi kipaumbele chao ni kufanya kazi na Serikali ili kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2025, Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano na Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo yamefafanuliwa katika Agenda ya Mwaka 2030.

Sekta ya madini yasaidia kuinua uchumi wa nchi
DJ D Ommy Afunguka Alivyowaunganisha Baraka Da Prince, Jux Na Ben Pol