Mkuu wa Wilaya ya Geita Mjini, Herman Kapufi  amewataka waandishi wa habari kuandika habari zenye ubora na zenye kuleta chachu ya maendeleo katika jamii.

Ameyasema hayo jana katika maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari yaliyofanyika ki mkoa mjini Geita ambapo yalihusisha wadau mbalimbali wa habari.

Amesema kuwa tasnia ya habari ni muhimu sana kulingana na kazi kubwa ya kutoa habari mbalimbali kwa jamii, hivyo amewaasa kuitendea haki taaluma hiyo kwa kutoa habari bila kuegemea upande mmoja.

Aidha, amewataka kuendeleza ushirikiano na taasisi mbalimbali ili kuweza kuibua changamoto ambazo zitasaidia kuleta maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Geita, Daniel Limbe amempongeza mkuu wa Wilaya ya Geita Pamoja na wadau wengine kwa kutoa ushirikiano wa bega kwa bega katika kuwasaidia waandishi ambao wapo wilayani humo.

 

 

Pablo Fornals Kurithi Mikoba Ya Santi Cazorla
Lukuvi ageuka 'mbogo' amsimamisha kazi afisa mipango miji Lindi