Kiungo wa Malaga CF, Pablo Fornals amesitisha kwa muda mpango wa kujiunga na Valencia CF baada ya kupata taarifa za klabu ya Arsenal, ambazo zimemshawishi kuitamani The Gunners kuelekea msimu wa usajili wa majira ya kiangazi.

Arsenal wameorodhesha jina la kiungo huyo, kwa lengo la kutaka kumsajili ili azibe nafasi ya Santi Cazorla ambaye huenda akaachwa mwishoni mwa msimu huu.

Hivi karibuni, Fornals mwenye umri wa miaka 21 aliripotiwa kuwa kwenye mazungumzo na Valencia CF ambao ni wapinzani wakubwa wa Malaga CF, lakini taarifa kutoka nchini Hispania zinasema kiungo huyo amesitisha kwa muda mazungumzo hayo ili kuona kama Arsenal watatimiza lengo la kutuma ofa ya kumsajili.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ameripotiwa kuwa kwenye msako mkali wa kuziba nafasi ya Cazorla, na tayari ameona Fornals mwenye mabao sita msimu huu kama mtu sahihi wa kukiongezea nguvu kikosi chake.

Kwa mujibu wa habari kutoka gazeti la michezo la Plaza Deportiva, Arsenal inaweza kumpata Fornals kwa dau dogo la Pauni milioni 10.

Ikiwa Arsenal itafanikiwa kumsajili Fornals itakuwa imefikisha wachezaji watatu waliowahi kuchezea Malaga CF. Wengine ni Santi Cazorla na Nacho Monreal.

Wakili Akabiliwa na Kifungo Cha Miaka 150 Jela Kwa Kumkashfu ‘Mfalme’
DC Kapufi awafunda waandishi wa habari Geita mjini