Kiungo wa klabu ya Hull City, Kamil Grosicki ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa nne (April) wa ligi kuu ya soka nchini England.
Grosicki kutoka nchini Poland ameshinda tuzo hiyo baada ya kupata kura 61,181 na kuwashinda Roberto Firmino wa Liverpool aliyepata kura 10,368 na Eden Hazard wa Chelsea aliyepata kura 9,539.Jumla ya kura zote zilizopigwa ni 97,000.
Wengine waliokua wanashindanishwa katika tuzo ya mwezi Aprili ni Christian Eriksen wa Tottenham aliyepata kura 8,346, Christian Benteke wa Crystal Palace aliyepata kura 4,065 na Dele Alli wa Tottenham aliyepata kura (3,988).
Mwezi Aprili Grosicki mwenye umri wa miaka 26, alitoa pasi tatu za mabao na kuiwezesha Hull City kupata ushindi dhidi ya kilabu za West Ham United, Middlesbrough na Watford