Mchezaji wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa anakipiga na timu ya Mbeya City, Mrisho Ngassa, amesema kuwa bila kujali kama alishawahi kuichezea timu hiyo ataikung’uta kama kawaida katika mchezo wao unaotarajiwa kuchezwa siku ya jumamosi.
Ngassa amesema kuwa mafanikio makubwa ya soka aliyoyapata kwa kiasi kikubwa yalichangiwa na klabu hiyo ya Jangwani, huku akisisitiza kuwa itakuwa ngumu kwake kushangilia bao endapo atafunga.
“Mpira ni kazi yangu na sasa nipo na Mbeya City ndio waajiri wangu naipenda timu yangu na nitahakikisha tunafanya kila liwezekanalo kuwafunga Yanga, lakini siwezi kushangilia nikifunga bao,” amesema Ngassa.
Hata hivyo, Kiungo huyo amesisitiza kuwa ili kuweka heshima ni lazima awafunge Yanga, huku akiwataka Wanajangwani hao kutotegemea mteremko kutoka kwao Jumamosi.