Ziara ya Rais wa Afrika kusini inchini imezaa matunda mara baada ya kusainiwa kwa mikataba mitatu ya ushirikiano katika sekta mbalimbali zitakazosaidia kukuza uchumi wa nchi hizo mbili, mikataba hiyo imesainiwa Ikulu jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa marais Dkt. John Magufuli na Jacob Zuma.

Nchi hizo mbili zimesaini hati ya muhtasari wa makubaliano ya mkutano wa tume ya pamoja ya Marais kati ya Tanzania na Afrika Kusini uliolenga kuboresha makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mkutano huo.

Mikataba mingine ni hati ya makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya Bi Anuwai kati ya Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini, inayolenga kuboresha ushirikiano katika sekta ya wanyamapori na uhifadhi, na mkataba wa tatu ni hati ya makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya uchukuzi kati ya Serikali ya Tanzania na Afrika kusini uliolenga kuboresha sekta ya uchukuzi.

Hata hivyo, katika mkutano huo Rais Magufuli amesema ziara ya Rais Zuma imekwenda sambamba na mkutano wa kwanza wa tume ya Marais ambapo umebainisha baadhi ya maeneo ya makubaliano.

 

Ngassa atamba kuitandika Yanga
Serengeti Boys yazidi kuneemeka na misaada