Magari zaidi ya 15,000 yamekamatwa jijini Dar es salaam na Kampuni ya Yono Auction Mart kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya mikopo na ukwepaji kodi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Scolastica Kevela alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa magari yote yaliyokamatwa ni yale ambayo yameshindwa kulipiwa kodi hivyo wao kama Wakala wa TRA kazi yao ni kuweza kukamata mpaka mdaiwa atakapolipa.

Amesema kuwa endapo wamiliki wa magari hayo na mizigo iliyokamatwa hawataenda kwa muda uliopangwa kulipa kodi wanazodaiwa, basi vitu na mali zao zitapigwa mnada.

“Niwaombe wananchi pindi magari yao yanapokamatwa au mizigo wanatakiwa kulipia kodi haraka kwani yanapozidi kukaa kwenye magodauni, na gharama nayo inaongezeka,”amesema Kevela.

Bob Marley atimiza miaka 36 tangu afariki dunia
Video: Chama cha ACT-Wazalendo chafanya mabadiliko makubwa ya uongozi