Nchi sita za Kiarabu ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia na Misri zimefunga uhusiano wa kidiplomasia na Qatar zikiituhumu kwa kuchochea uvunjifu wa amani na kuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi ya Al-Qaeda na kundi linalojiita Islamic State of Iraq and Syria (ISIS).
Shirika la habari la Saudi la SPA limeeleza kuwa Riyadh amefunga mipaka yote ya ardhini na mawasiliano ya anga na kibiashara kati yake na Qatar.
Hata hivyo, Qatar imepinga vikali uamuzi huo ikidai kuwa ni uamuzi usio wa kiungana na kwamba hawajatendewa haki. Imeongeza kuwa tuhuma za kuhusishwa na makundi hayo ya kigaidi ni za kutungwa na hazina ukweli wowote.
Tamko la Saudi pia limeihusisha Qatar na makundi ya kigaidi yenye makazi yake nchini Iran, nchi ambayo imekuwa na mgogoro nayo.
Uamuzi huo wa kufunga milango ya kidiplomasia dhidi ya Qatar ilianza na Bahrain kisha Saudi Arabia ikafuata mapema leo. Wengine ni Libya, Yemen, Misri na Falme za Kiarabu.