Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa agizo kwa Jeshi la Polisi nchini kuyaachia magari yote ambayo yanashikiliwa na Jeshi hilo kwa kosa la kutolipia ada ya mwaka ya leseni ya magari.
- Video: Serikali yafuta ada ya mwaka leseni ya magari, yatoa msamaha wa kodi, riba
- Video: Dkt. Mpango aondoa ushuru kusafirisha mazao yasiyozidi tani 1
Waziri Mwigulu ametoa agizo hilo baada ya Serikali kufuta ada hiyo ambayo italipwa mara moja tu gari litakaposajiliwa.
Serikali imetangaza kufuta ada hiyo pamoja na kutoa msamaha wa kodi, riba na adhabu zinazoambatana na madeni yote (Tax Amnesty) ya ada hiyo yaliyolimbikizwa kwa miaka ya nyuma.