Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefuta ada ya mwaka ya leseni ya magari na badala yake ada hiyo italipwa mara moja tu gari litakaposajiliwa.

Hayo yamesemwa na Serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2017/18 Bungeni Dodoma, ambapo amesema kuwa baada ya kufutwa kwa ada hiyo baada ya hapo itaendelea kulipwa kupitia Ushuru wa Bidhaa kwenye mafuta ya petroli na dizeli kwa kuongeza Ushuru wa Bidhaa kwenye mafuta ya petroli, dizeli na taa.

Dkt. Mpango amesema kuwa Serikali pia inatoa msamaha wa kodi, riba na adhabu zinazoambatana na madeni yote (Tax Amnesty) ya ada hiyo yaliyolimbikizwa kwa miaka ya nyuma.

Kufuatia hayo, Serikali itaongeza Ada ya Leseni ya Magari wakati wa usajili mara ya kwanza (Annual Motor Vehicle Licence Fee on first registration), ambapo ongezeko litakuwa ni kiasi cha shilingi shilingi 50,000 kwa gari lenye ujazo wa injini ya 501-1500 cc yaani kutoka kiwango cha sasa cha shilingi 150,000 hadi shilingi 200,000; gari lenye ujazo wa injini ya 1501-2500 cc kutoka kiwango cha sasa cha shilingi 200,000 hadi shilingi 250,000, ikiwa ni ongezeko la shilingi 50,000; na

Gari lenye ujazo wa injini ya 2501 cc na zaidi kutoka kiwango cha sasa cha shilingi 250,000 hadi shilingi 300,000, ikiwa ni ongezeko la shilingi 50,000.

Hatua hizi kwa pamoja zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 77,603.5

Nicki Minaj aahidi mapinduzi ya hip hop kwa mzigo huu
Video: Dkt. Mpango aondoa ushuru kusafirisha mazao yasiyozidi tani 1