Baada ya sakata la muda mrefu la tuhuma za rushwa linalomkabili Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, hatimaye Jaji Mkuu nchini Brazil ameagiza kushikiliwa kwa mali za Rais huyo baada ya kukutwa na hatia ya rushwa.
Jaji Mkuu wa nchi hiyo, Sergio Moro amesema kuwa kiasi cha dola za Marekani laki mbili zimegunduliwa katika akaunti ya kiongozi huyo wa zamani, hivyo kupelekea kushikiliwa kwa mali anazomiliki yakiwemo maghorofa matatu , ardhi kubwa ambayo alijimilikisha na magari mawili ya kifahari.
Aidha, Rais huyo wa zamani aliyejipatia umaarufu wa kuwatumikia wananchi wake kwa kuweka sera ya kuwajali wanyonge, alitumia fursa hiyo kuweza kujitajirisha kwa kuiba mali za umma.
Hata hivyo, Da Lula ataendelea kuzitumia mali zake hizo endapo atashinda katika rufaa yake aliyoikata ya kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama nchini humo ya kwenda jela miaka tisa na nusu iliyotokana tuhuma za rushwa.
-
Rais wa zamani wa Brazil ahukumiwa kwenda jela miaka tisa na nusu
-
Rais wa Brazil kikaangoni, Bunge lamkingia kifua
-
Putin, Trump wateta kwa siri mkutano wa G20
-
Winnie Mandela aishukia serikali ya Afrika Kusini
Rais huyo wa zamani wa Brazil, hivi karibuni alihukumiwa kwenda jela miaka tisa na nusu mara baada ya kukutwa na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na tuhuma za rushwa ambazo zilikuwa zikimuandama.