Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, ameyaponda matamko yaliyotolewa na mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu, amesema kutaka nchi kunyimwa misaada ni uhayawani, kwani vita dhidi ya kuminywa kwa demokrasia inapaswa kupiganiwa ndani.
Zitto alitoa kauli hiyo kupitia akaunti yake katika Mtandao wa Kijamii wa Twitter, ikiwa ni siku moja tu baada ya Chadema kupitia kwa mwanasheria wake, Tundu Lissu kuitaka Jumuia ya Kimataifa kuinyima Tanzania misaada kufuatia kitendo cha kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa viongozi wa upinzani, hasa kutoka chama chao.
-
Mambosasa: Hatuna mpango wa kumkamata Lissu
-
JPM atoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vya mafuta nchini
“Huu ni uhayawani, hii ni nchi huru, kukaribisha wageni kuingilia mambo yetu ni upuuzi na umazwazwa, tupambane ndani kuleta demokrasia,” ameandika Zitto.
Hata hivyo, kufuatia kauli hiyo baadhi ya watumiaji wa mtandao huo walianza kumuuliza maswali kadha Zitto ambaye aliwajibu na kuufanya mjadala huo kuwa mrefu, baadhi wakimuunga mkono na wengine wakipingana naye.