Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ilitoa taarifa juu ya kuanza majadiliano baina ya kamati Maalumu iliyoundwa na Rais John Magufuli na Wawakilishi kutoka kampuni ya Barrick Gold Corporation juu ya biashara ya madini yanayochimbwa na kampuni hiyo.

Hatua iliyofikiwa hadi sasa ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuitaka kampuni hiyo kulipa deni la mapato iliyojilimbikizia tangu mwaka 2000, ambapo hadi sasa Tanzania inadai kampuni hiyo dola za kimarekani milioni 90 ambayo ni sawa na shilingi trilioni 420 za kitanzania.

Ambapo deni hilo limeweza kunyumbuliwa na kubainika kuwa endapo litalipwa basi Serikali inauwezo wa kufanya mambo yafuatayo kwa watanzania.

1. Kuwezesha ununuaji wa gari aina ya Noah kwa kila Mtanzania mwenye umri juu ya miaka 18

2. Kujenga mtandao mkubwa zaidi wa barabara za lami

3. Kugawa mtaji wa biashara ya kiwango cha zaidi ya milioni 10 kwa kila mwanamke nchini.

4. Kusomesha bure idadi kubwa ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa takribani miaka 5.

5. Kuwanywesha watoto wenye chini ya miaka 15 angalau lita tatu za maziwa kila siku mwaka mzima.

6. Kuwanunulia bajaji na pikipiki watanzania wote.

7. Kujenga mahabara shule zote za serikali Tanzania, na kuwezesha kununua mamilioni ya madawati

8. Kutoa dawa bure kwa kila mtanzania kwa takribani miaka 20 mfululizo.

9. Kuwanunulia kreti la bia wanaume wote kwa mfululizo wa miezi saba.

Hivyo unyumbulifu huo wa deni la malimbikizo ya fedha toka kampuni ya Barrick Gold Corporation unamfanya kila mtanzania kuwa na sababu ya kutanguliza sala na maombi kwa kamati iliyoundwa ili ifanye vizuri kufanikisha deni hilo kurejeshwa nchini.

 

JPM awataka wapinzani mkoani Tanga kutojisifia
JPM awaunganisha Ruge na Makonda jukwaani, ‘nataka mpendane’