Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda imemtangaza Rais wa nchi hiyo, Paul Kagame kuwa mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika tarehe 4 Agosti mwaka huu ncjhini humo.

Tume hiyo imesema kuwa matokeo ya awali yameonyesha kuwa Rais Kagame ameongoza kwa kwa asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa, hivyo kumpa nafasi kubwa ya kuendelea kuongoza nchi hiyo.

Aidha,  Rais Kagame ambaye amekuwa madarakani kwa miaka kumi na saba sasa ataendelea kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu mfululizo ambapo Katiba ya nchi hiyo inamruhusu kuongoza kwa miaka saba.

Rais Kagame aliingia madarakani mwaka 1994 wakati kundi lake la waasi lilipoudhibiti mji mkuu Kigali na kukomesha mauaji ya kimbari ambapo watu 800,000 Watusi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa.

Hata hivyo, Wapinzani wa Kagame wamelalamika kuwa wafuasi wao wanahangaishwa na kunyanyaswa huku wakisema kuwa ndiyo sababu kubwa ya wapinzani hao kutojitokeza kupiga kura.

LIVE: Rais Magufuli, Museven katika uzinduzi wa bomba la mafuta Tanga
Wakuu wa shule wapewa mbinu za kuongeza ufaulu