Shirika la kutetea haki za Wanyama nchini Kenya limesema kuwa nyama ya punda imepanda bei mara dufu nchini humo kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya nyama ya Punda nchini China nchi ambayo hununua kwa wingi nyama hiyo.

Shirika hilo limesema kuwa nyama ya mnyama huyo imepanda kutokana na nchi ya China kuongeza kiwango cha uhitaji wa nyama ya Punda nchini humo hivyo kupelekea kuadimika kwa mnyama huyo.

Bei ya Mnyama huyo imepanda na watumiaji nchini humo wamesema kuwa Mnyama huyo amekuwa adimu kutokana China kuongeza mahitaji ya nyama ya Punda ambayo ndiyo kitoweo kikubwa katika nchi hiyo.

Aidha, baadhi ya Mataifa barani Afrika yamepiga marufuku uuzaji ya nyama na bidhaa nyinginezo za punda, nchini China kwa sababu mnyama huyo hutumiwa zaidi kwa ajili ya kusaidia kubeba mizigo mashambani, sasa idadi yao inapungua kwa kasi kubwa.

Hata hivyo, Baadhi ya Mataifa ya Afrika yaliyopiga marufuku uchinjaji na uuzaji wa nyama ya Punda ni pamoja na Uganda, Tanzania, Botswana, Niger, Burkina Faso, Mali, na Senegal.

Meya wa Ubungo ateta na machinga, awataka kupisha ujenzi wa 'Flyover'
Magazeti ya Tanzania leo Agosti 31, 2017