Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka na aliyekuwa Kaimu Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha ambaye ni Askofu wa Kanisa la Pentecoste Motomoto, Elisaph Mathew kwenda jela miaka sita ama kulipa kiasi cha shilingi milioni 35 kwa kila mmoja.

Wawili hao wamehukumiwa kifungo hicho kutokana na mashtaka yao sita waliyokuwa yanawakabiri pia Mahakama imewataka washtakiwa hao kulipa hasara waliyoisababishia ATCL kwa kununua magari chakavu 26, yaliyokuwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 143 ndani ya mwezi mmoja.

Aidha, kwa upande mwingine, Mahakama imemuachia huru William Haji aliyekuwa mkaguzi mkuu wa hesabu za ATCL kutokana na kesi yake kufutwa hivyo ameachiwa huru ili aweze kuendelea na shughuli zake za kila siku.

Hata hivyo, watuhumiwa hao kwa ujumla walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kulisababishia hasara Shirika la Ndege la Tanzania, ATCL hivyo kutakiwa kurejesha gharama zote walizolisababishia shirika hilo.

 

Wanamgambo 6 wa Al-Shabaab wauawa
Spika Ndugai awatwisha zigo wabunge wanawake