Kufuatia ajali ya moto iliyotokea kwenye makazi ya Jeshi la Polisi mkoani Arusha September 27, 2017 majira ya saa moja na Nusu usiku, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelipatia jeshi hilo Milioni 260 kwa ajili ya kujenga nyumba hizo.

Akizungumza na Waandishi ya Habari, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro amesema kuwa Rais Magufuli ametoa fedha hizo kutokana ya ajali ya moto iliyotokea jana na kusababisha  familia za askari wa polisi 14 na zenye wakazi 44 kupoteza mali na makazi ya kuishi.

Sirro amesema kuwa Jeshi Polisi Tanzania limetoa kiasi cha shilingi milioni 40 kutoka kwenye mfuko wa Jeshi hilo ili kusaidia kujenga makazi mapya ndani ya mwezi Mmoja na kuzipatia milioni moja kila familia ya askari hao ili kuweza kujikimu kimaisha.

“Rais ameagiza wakala wa Taifa wa majengo (TBA) kuwapatia askari makazi mpaka hapo ujenzi utakapokamilika ndipo waweze kurejea kwenye makazi yao ya kudumu” amesema Sirro

IGP Sirro amewasisitiza Askari polisi kuwa ajali hiyo iliyotokea ni kama ajali zingingene hivyo waendelee kuwa na imani na serikali wakati wanashughulikia jambo hilo kukamilika mapema ndani ya Mwezi mmoja.

Aidha, IGP Sirro amewaomba Raia wema na Taasisi za Watu Binafsi kujitokeza kutoa msaada kwa wahanga wa tukio la kuunguliwa na nyumba zao na kupoteza mali zao zenye thamani kubwa.

 

Video: INAUMA SANA! Binti mwenye ugonjwa wa ajabu asimulia mazito, apaza sauti kuokoa maisha yake

Magazeti ya Tanzania leo Septemba 29, 2017
Amuua mwenzake kisa mabishano kuhusu makalio ya mwanamke