Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, limemshikilia mkazi wa Katoro, Hapiness John (22), kwa kusababisha vurugu baada ya kudai kuwa ana uwezo wa kumfufua mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Juma Charles (25), ambaye amefafiki Novemba, mwaka jana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, amesema katika Mtaa wa Bugayambilele ambako mtuhumiwa ni mpangaji wa mama wa marehemu, alidai kuwa Charles hajafariki dunia na kwamba amewekwa msukule na jirani yake, Rebeca Lusana (mama Latifa) ambaye ni fundi cherehani mtaani hapo.
-
Shonza amfungia msanii Pretty kujihusisha na sanaa kwa miezi sita.
-
Muisrael akamatwa kwa kuuza viungo vya Binadamu
Ambapo mwanafunzi huyo alikufa kwa ajali ya gari na kuzikwa pembeni ya nyumba yao, na vurugu ilianza baada ya mtuhumiwa kuonekana akinyunyizia dawa za kienyeji kwenye kaburi la marehemu huku akiongea maneno yasiyoeleweka, akidai kuwa anamfufua marehemu huyo.
Na mtuhumiwa uyo aliwahakikishia kuwa kijana Charles bado yupo hai na anatembea mtaani kila siku.
Hivyo Polisi ilimshika mtuhumia huyo na kumtaka awapeleke alipo marehemu ili wakamchukue, jambo hilo lilizua vurugu na umati wa watu.
Kamanda Mwabulambo, alisema mtuhumiwa bado anashikiliwa na polisi hadi uchunguzi utakapokamilika na akikutwa na hatia atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kuwa na nia ya kuvunja amani na kutoa taarifa ya uongo.