Ugonjwa wa mlipuko wa kipindupindu umeendelea kuleta athari kubwa nchini Zambia tangu mwishoni mwa mwaka jana, na sasa umesababisha ibada kusitishwa katika maeneo kadhaa nchini humo.

Maafisa wa afya nchini humo wameliambia shirika la habari la BBC kuwa idadi ya watu wenye kipindupindu inazidi kuongezeka na hadi jana walikuwa wamefikia 2,451, idadi kubwa zaidi ikiwa jijini Lusaka.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, watu 61 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo na kwamba kati ya hao 58 walikuwa wakaazi wa jiji la Lusaka.

Baadhi ya makanisa yametangaza kusitisha kwa muda huduma za ibada, ikiwa ni pamoja na makanisa makubwa ya ‘Reformed Church in Zambia’ na ‘The Bread of Life Church International’.
Aidha, sekta ya elimu ilikuwa ya kwanza kuathiriwa na kuwepo kwa ugonjwa huo wa mlipuko ambapo Waziri wa Afya, Dkt. Chitalu Chilufya akishirikianana wizara ya elimu alitangaza kuahirishwa kwa ratiba za masomo hadi itakapotangazwa tena.

“Kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu tangu Oktoba mwaka jana, ambao umeathiri maeneo mengi ya Lusaka, tumeanza kuona hali hiyo katika maeneo mengi ya nchi,” alisema Dk. Chilufya.

Rais wa Zambia, Edgar Lungu aliagiza Jeshi la nchi hiyo kuingia mitaani kushirikiana na wizara husika kuhakikisha wanasaidia katika hatua za kuondokana na ugonjwa huo.

Atiwa mbaroni kwa kutaka kumfufua mfu
Magazeti ya Tanzania leo Januari 8, 2018