Watu 13 wameuawa kwa kupigwa risasi Kusini mwa Senegal, katika mkoa wa Casamance.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na uongozi wa hospitali iliyopokea miili hiyo, waliouawa kwa risasi walikuwa vijana wenye umri chini ya miaka 20.
Jeshi la Senegal limeeleza kuwa miili hiyo ilikutwa katika maeneo ya vichakani na kwamba vijana hao walikuwa wanatafuta kuni kwa ajili ya kupikia. Jeshi hilo limeeleza kuwa ingawa hakuna kundi lililoeleza kuhusika na shambulizi hilo, waasi wa MFDC wanahusishwa zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa za jeshi hilo, tukio hilo linaweza kuwa na uhusiano na kuachiwa kwa hivi karibuni kwa wanamgambo wawili wa MFDC.
Eneo la Casamance limekuwa na mgogoro mkubwa kati ya Serikali na waasi wa MFDC ambao wanadai uhuru wa eneo hilo. Maelfu ya watu wameuawa kutokana na mgogoro huo tangu mwaka 2014.