Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa la nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 22 na 23 mwaka jana, huku ikionesha idadi kubwa ya wanafunzi wamefanya vizuri mitihani hiyo.
Matokeo yametangazwa leo Jumatatu Januari 8,2018 na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo.
-
MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI 2017
-
MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE 2017
Aidha ameeleza kuwa wanafunzi wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D na wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha.
Kuhusu matokea ya upimaji wa kidato cha pili, Dk Msonde amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.
Dk Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili 51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.