Msanii ambaye hana muda mrefu tangu aliposainiwa na lebo ya WCB, amevuma na kupjipatia umaarufu wake kupitia kibao cha tuachane, Lava Lava amekuja na video mpya ya “Kilio” ikiwa ni siku mbili zimepita tangu aachie video ya ‘Teja’.

Lava Lava ambaye hivi karibuni amejiunga na kundi hilo amekuwa akifanaya vizuri kazi zake za sanaa ya muziki akishirikiana na wasanii  wengine kutoka kwenye kundi hilo.

Mbali na msanii huyo kusajiliwa katika kundi hilo, Maromboso ambaye alikuwa katika kundi la Yamoto Bendi, mara baada ya kundi lake kuvunjika amesajiliwa chini ya WCB na anafanya kazi chini yakundi hilo, ila cha kushangaza ni kwamba bado kazi zake yeye  kama yeye hazijaanza kuonekana.

Mara ya mwisho Maromboso kufanya kazi ilikuwa ni wimbo wa Zilipendwa ambao ulijumuisha wasanii wote chini ya lebo hiyo ya WCB.

Mashabiki wanahoji na wanataka kusikia kazi za Maromboso kwani kazi za kina Beka, Aslay ambao hawana mameneja wa kuwasimamia zinasikika na kupendwa na wengi, wamehoji Maromboso aache kuonekana katika video za watu afanye kazi bila hivyo atapoteza mashabiki wake.

Kuutazama wimbo Lava Lava bonyeza lonk hapo chini.

Necta yatangaza matokeo kidato cha pili na darasa la nne
Watakaosimama na wanafunzi wa kike kukumbana na hili