Brown ambaye alikuwa mpenzi wa mwanamitindo na mcheza filamu Bongo , Jackline Wolper amefunguka na kuweka wazi sababu ya kuachana na mpenzi wake huyo na kusema yeye ndiye alimkosea  na kila alipoomba msamaha Wolper hakutaka kumuelewa.

Brown alipohojiwa hakutaka kuueleza alichomkosea aliyekuwa mpenzi wake Wolper kwani anaamini kuwa ugomvi huo ulikuwa baina yao wawili na ikiwa tayari wameshaachana haoni sababu ya kuelezea nini hasa alimfanyia.

Zaidi Brown ameweka wazi kuhusiana na picha zilizovuja mtandaoni  akiwa na mwanamke mwingine, ambapo mashabiki walihisi ndiyo chanzo cha wawili hao kuachana.

Brown amesema picha hizo hazihusiani na ugomvi huo wala kuachana kwao kwani tangu wawili hao waachane yapita mwezi sasa.

”Aliyevujisha picha hizo aliona ni wakatai muafaka wa yeye kuvujisha kwani tayri nilikuwa nimeachana na Wolper” amesema Brown.

Mara baada ya kuachana na kijana huyo maarufu kamaBrown, Wolper amekuwa akipost katika mitandao yake ya kijamii akitambulisha matukio yake ya kuvalishwa pete na matukio mengine kuelekea tendo zima la ndoa na mwanaume amabaye hakutaka kumeweka wazi.

Kupitia mtandao wa snapchat pamoja na instagram Jacquline Wolper amepost picha ambazo zinaashiria kuwa ameshaolewa kutokana na captions alizoziandika.

 

Video: JPM amteua kamishina mwingine wa madini
Jela kwa kuoa mama na binti yake