Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema kuwa raia wa Syria wanapaswa kushikamana na kuwa na maono ya pamoja juu ya mustakabali wao wa baadaye ili kukabiliana na mgogoro unaoendelea nchini mwao.

Akisoma hotuba kwenye mkutano huo kwa niaba ya Rais Putin, Waziri wa mambo ya nje wa Urusi. Sergei Lavrov amesema kuwa kuna mikakati imewekwa kwa ajili ya kufungua ukurasa mpya katika historia ya Syria, akisema ni Wasyria wenyewe ndio wanaoweza kuamua mustakabali wa nchi yao.

Aidha, Lavrov amezishukuru Uturuki, Iran na Umoja wa Mataifa kwa kuunga mkono mazungumzo ya amani ya Syria ambayo yatasaidia kuondokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Baadhi ya wajumbe katika mkutano huo walisimama na kumzomea Sergei Lavrov wakati alipokuwa anatoa hotuba yake, wakiituhumu Urusi kuhusika na mauaji ya raia nchini Syria kwa mashambulizi yake ya angani nchini humo.

Hata hivyo, tukio hilo pia lilionyeshwa moja kwa moja kupitia televisheni ya Taifa ya Urusi ambapo maafisa wawili walionyeshwa wakimfuata mtu mmoja katika mkutano huo na kumtaka akae chini na kunyamaza.

Wakimbizi 1200 wa DRC waingia Tanzania
Wapinzani wagoma kutoa maoni Bungeni