Mwendesha mashtaka nchini Niger ameiomba mahakama nchini humo iwape adhabu ya kifungo kisichopungua miaka 20 jela wanaume kumi wanaotuhumiwa kutaka kumteka Rais Mahamadou Issoufou.

Kwa mujibu wa mashtaka yaliyowasilishwa mahakamani hapo, kundi hilo la watu linaloundwa na wanajeshi tisa pamoja na raia mmoja lilipanga kumteka Rais Issoufo Disemba 18 mwaka 2015 akiwa na kiongozi wa kikosi cha ulinzi wa Rais.

Taarifa za kipelelezi zilieleza kuwa kama wawili hao wangekataa kutekwa, watu hao walikuwa wamepanga kuwaua mara moja.

Aidha, zaidi ya watu 20 walikamatwa katika jaribio lingine lililotangazwa na Serikali kuwa la kufanya mapinduzi lakini baadhi yao waliachiwa mwezi Machi mwaka huu.

Rais Mahamadou Issoufou

Kambi ya upinzani nchini humo inaeleza kuwa matukio yote hayo yametengenezwa na Serikali kwa sababu za kisiasa.

Timu ya waendesha mashtaka nchini humo pia inaiomba Mahakama kumpa adhabu kali Souleymane Salou ambaye alikuwa mfanyakazi wa karibu wa Rais kwa madai ya kupanga uhaini mwaka 2010.

DC Polingo amsweka ndani mkandarasi
Taasisi za umma zatakiwa kutumia gesi