Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kurudi salama kutoka nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu.
Ameyasema hayo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akielezea maendeleo ya hali yake, ambapo amesema kuwa ilifikia kipindi akawa anaona hapakuchi.
Amesema kuwa hawaombei Wabunge wapitie hali aliyoipitia bali anawaombea wasipitie machungu ambayo yeye yalimpata.
“Baadhi yenu labda hamjawahi kulazwa hospitali mkiwa mnaumwa sanaa halafu somehow ukawa pekee yako unaweza kuona Kuna wakati fulani mawazo yanavyokuja yanavyozunguka na wakati mwingine dalili zilikuwa zinataka kuonyesha kama kesho kunaweza kusikuche hivi, ina raha yake na tabu yake kidogo. Siwaombei mpitie katika mambo hayo nawaombea msipate machungu hayo,”amesema Ndugai
Aidha, Ndugai amewapongeza wasaidizi wake wakiongozwa na Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson na Katibu wake pamoja na wabunge wote kwa ujumla na kuwaomba waendeleze gurudumu kwani kipindi kinachofuata ni kirefu sana cha Bunge la Bajeti.
-
Video: Serikali yawarejesha kazini watumishi waliokuwa wamefukuzwa
-
Video: Dar24 Media yatoa elimu kuhusu madhara ya dawa za kulevya
-
Waziri Mkuu awataka mabalozi kutangaza vivutio vya uwekezaji nchini
Hata hivyo, amewashukuru wale wote waliomuombea na kumjulia hali alipokuwa kwenye matibabu hususani Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliyekuwa akimjulia hali mara kwa mara pamoja na Wananchi wa jimbo lake (Kongwa).