Afisa Mwandamizi wa Korea Kaskazini anayetajwa kuwa mtu wa karibu zaidi wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un ameweka historia ya kuwa kiongozi wa kwanza mzito zaidi wa nchi hiyo kuwasili nchini Marekani katika kipindi cha zaidi ya miaka 20.

Gen Kim Yong-chol ambaye alikuwa katika orodha ya maafisa wa Korea Kaskazini waliopigwa marufuku kukanyaga ardhi ya Marekani, jana alitua jijini New York na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo.

Pompeo alitumia mtandao wa Twitter kuthibitisha kufanyika kwa mkutano kati yake na Gen Kim na kwamba wanaweza kukutana tena leo.

Viongozi hao walifanya mazungumzo na kupata chakula cha usiku pamoja, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kufanikisha mkutano wa kihistoria kati ya Rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un.

Wiki iliyopita, mkutano huo uliingia mashaka baada ya Trump kutangaza kuwa umeahirishwa.

Gen Kim Yong-chol ni kiongozi wa ngazi za juu zaidi wa Korea Kaskazini kuitembelea Marekani katika kipindi cha miaka 20 iliyopita kutokana mgogoro wa silaha za nyuklia kati ya mataifa hayo.

Trump na Kim wanatarajia kukutana Juni 12 mwaka huu na endapo mkutano huo utafanikiwa utaweka historia ya marais walioko madarakani wa nchi hizo kukutana kwa mara ya kwanza.

Awali, moja kati ya doa lililodondoka kwenye shuka jeupe la jitihada za mkutano wa viongozi hao ni pale Korea Kaskazini ilipojibu kwa kulaani vikali kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kufananisha hatma ya Korea Kaskazini na Libya katika kuachana na mpango wa silaha za nyuklia.

Tayari Korea Kaskazini imeanza kuchukua hatua kwa kuharibu maeneo ya kufanyia majaribio silaha zake za kinyuklia.

Mhubiri awaomba waumini wamnunulie Ndege
Fahamu mambo 5 juu ya urembo hapo kale