Mhubiri mmoja wa Injili nchini Marekani, Jesse Duplantis amewaomba waumini wake kuchanga pesa za kumsaidia kununua ndege yake ya nne.

Amesema kuwa hata kama Yesu angekuwepo siku hizi, asingeweza kupanda punda kama alivyokuwa akipanda hapo zamani.

Jesse Duplantis amesema kuwa Mungu amemwambia anunue ndege aina ya Falcoln 7X ambayo inagharimu $54m (£41m).

“Mnajua, nimemiliki ndege tatu maishani mwangu, na nimezitumia na kuchoma mafuta kwa ajili ya Bwana Yesu Kristo, hivyo kwasasa nawaombeni mninunulie ndege mpya, ingawa baadhi ya watu wanaamini kwamba wahubiri hawafai kuwa na ndege,”amesema Duplantis

Hata hivyo, Duplantis ametetea ombi lake la kutaka kununuliwa ndege akisema Yesu aliwaambia wafuasi wake “nendeni kote duniani na mkahubiri Injili kwa kila kiumbe, sasa tutawezaje kutimiza hilo? amesema kuwa hawezi kuishi muda mrefu wa kutosha kusafiri kote kwa kutumia gari au meli au treni, lakini anaweza kusafiri mbali kwa kutumia ndege.

Picha: Kim Kardashian ateta na Trump Ikulu
Kigogo mzito wa Korea Kaskazini aweka historia Marekani