Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika majimbo matatu na wa udiwani katika kata mbili za Tanzania Bara utakaofanyika Septemba 16, mwaka huu.

Akitangaza uchaguzi huo mjini Dodoma Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Mbarouk Salim Mbarouk amesema kuwa fomu za uteuzi wa wagombea wa Majimbo hayo zitatolewa kuanzia tarehe 13 hadi 20 Agosti mwaka huu na uteuzi utafanyika tarehe 20 Agosti, 2018.

Amesema kuwa kampeni zinatarajiwa kuanza Agosti 21 na kumalizika Septemba 15, mwaka huu.

“Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Ubunge katika Majimbo matatu,”amesema Jaji Mbarouk

Aidha, ameyataja majimbo hayo kuwa ni Korogwe Vijijini, Mkoa wa Tanga kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Stephen Hilary Ngonyani, Jimbo la Ukonga Katika Mkoa wa Dar Es Salaam na Jimbo la Monduli katika Mkoa wa Arusha

 

Skimu za umwagiliaji kuinua uchumi wa viwanda nchini
Kigwangalla akimbizwa KCMC