Mwanamke mwenye asili ya Tanzania, Tanzeela Qambrani ameweka historia ya kuwa Mbunge wa kwanza mwenye asili ya Afrika akiiwakilisha jamii ndogo iliyotengwa ya Sidi iliyoko katika eneo la Markan na Karachi
Mababu wa Mwanamke huyo walihamia nchini humo kama watumwa karne moja iliyopita. Jamii ya Sidi au Sheedi au Habashi ni ya wahamiaji kutoka nchi za Maziwa Makuu (Afrika Mashariki).
Aidha, Tanzeela alipendekezwa kuwania nafasi hiyo kutoka katika chama (Pakistan Peoples Party) kilichotoa Waziri Mkuu wa kwanza Mwanamke, Benazir Bhutto
Hata hivyo, Wakati akihojiwa Tanzeela alieleza kuwa anayofuraha kupata nafasi hiyo kwani ataleta uwakilishi wenye tija katika bunge la nchi hiyo.
-
Trump aiwekea Zimbabwe ‘kisiki’ kingine kisa uchaguzi
-
UN yampongeza Rais Kabila, yahimiza uchaguzi wa amani na haki DRC
-
Majaliwa ahimiza ubobezi kwenye Sheria
Kuhusu asili yake, Tanzeela alieleza kuwa ni kweli anaasili ya Tanzania na hata Dada yake ameolewa Tanzania