Mwinyi mgeni rasmi maadhimisho siku ya Kiswahili Duniani
3 years ago
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewasili na kukagua Vikundi vya Wajasiriamali katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani ambayo kwa mara ya kwanza yanafanyika Visiwani Zanzibar.
Rais Dkt. Hussein Mwinyi, ni Mgeni Rasmi na mdau wa lugha ya Kiswahili katika kilele cha maadhimisho haya, na zifuatazo ni picha zinazomuonesha akikagua mabanda mbalimbali ya wanasiriamali katika eneo la Hotel ya Golden Tulip Airport Zanzibar.